1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Hungary nani kuibuka mbabe?

22 Juni 2021

Katika mchezo wa Ujerumani wa (23.06.2021) inaweza kujikatia tiketi ya kuingia katika hatua ya mchujo ya mashindano ya Kombe la Ulaya - Euro 2020, huku wenzao mabingwa watetezi Ureno wakiwa hatarini kuondoshwa.

Deutschland Fussballfans singen in Berlin
Picha: John Macdougall/AFP/Getty Images

Matarajio hayo yanajitokeza licha ya nyota wake Cristiano Ronaldo kuwa na mwanzo mzuri katika Kundi F. Ufaransa inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne kabla ya kucheza leo dhidi ya Ureno, ikiwa ishara ya kilichojitokeza katika fainali ya Euro 2016. Ujerumani na Ureno zote zina pointi kila mmoja baada ya rekodi za kufunga na kufungwa kwa kuitandika Ureno 4-2 katika mechi iliyopita.

Endapo kutatokea matekeo ya sare Ureno inaweza kupata tiketi ya kucheza hatua inayofuata kama moja ya timu nne bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu, kama tu ilivyokuwa kwao walipobeba taji hilo miaka mitano iliyopita nchini Ufaransa.

Ureno inautazamaje mchuano wa Ujerumani na Hungary 

Mchezaji wa timu ya Ureno, Cristiano RonaldoPicha: Darko Bandic/AP/picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Ureno ilianza kwa kishindo mchuano huo kwa kuichapa Hungary mabao 3-0, huku Ronaldo akiwa mfugaji anaeongoza katika historia ya mchuano wa mabingwa barani Ulaya. Kocha wa timu hiyo, Fernando Santos ambae timu yake ilichakazwa vibaya na Ujerumani Jumamosi iliyopita amesema ataufuatilia vyema mchuano huo, ili kujijengea uwezo na kujitambua kwamba nao watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Ufaransa.

Nae kiungo wa timu hiyo, Joao Moutinho amesema katika mchezo huo dhidi ya Ufaransa wana kazi ngumu ya kufuta taswira ya yaliopita.

Tembo wa Hamburg atabiri Ujerumani kutoka suluhu na Hungary

Tembo mmoja mwenye kuaminiwa kuwa na ufahamu mzuri wa katika bustani ya wanyama wa Hamburg, nchini Ujerumani ameonesha ishara kwamba Ujerumani itatoka suluhu na Hungary katika mchezo wake huo wa Munich. Tembo huyo aitwaye Yoshoda mwenye umri wa miaka 42, alizitoa bendera za Hungary kwenye boksi katika bustani hiyo ijulikanayo kama Hagenbeck Zoo.

Yoshoda aliwahi kutioa utabiri, ambao ulileta matokeo ya kweli pale alipoonesha ishara ya Ujerumani kushindwa dhidi ya Hatua ya makundi yakaribia mwishoUfaransa katika mchezo wake wa ufunguzi na pia kuichapa Ureno katika mchezo wake wa pili. Mkurugenzi Mtendaji wa Hagenbeck Dirk Albrecht amesema wanafurahi kwa utabiri wa tembo huyo na kwamba itakuwa faraja zaidi kama utabiri wake wa mara ya tatu utakuwa wa kweli.

Matokeo ya sare kwa timu ya Ujerumani yataiingiza timu hiyo katika hatua ya mtoano na Hungary kuondolewa kabisa katika mashindano hayo.

Mbali na mechi hiyo ya kundi F, mchuano mwingine wa kundi F, hapo 23.06.2021 utazikutanisdha Ureno na Ufaransa, kwa kundi E, Slovakia na Uhispania kwa upande mwingine Sweden na Poland.Lakini leo hii timu zinazoshuka dimbani kwa kupitia kundi D ni Jamhuri ya Czech na England pamoja na Croatia na Scotland.

Vyanzo: AFP/DPA