Ujerumani na Italia kufanya mkutano wa kilele Berlin
22 Novemba 2023Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni leo watakubaliana kushirikiana katika masuala ya nishati hadi ulinzi katika mkutano wa kilele utakaofanyika mjini Berlin.
Mkutano huo ndio wa kwanza kufanyika baina ya nchi hizo katika kipindi cha miaka saba. Mpango wa utendajiwa kurasa 31 utakaotiwa saini na viongozi hao wawili katika mkutano huo na ambao shirika la habari la Reuters limeona nakala yake, haujalipa kipau mbele suala la uhamiaji, licha ya kuwa mpango wa uhamiaji wa Ujerumani unaoana na ule wa Italia.
Soma pia:Nigeria na Ujerumani zatia saini makubaliano ya gesi na nishati mbadala
Katika mpango huo Ujerumani na Italia zinaahidi kuwa na majadiliano ya mara kwa mara, kwa mfano kupitia mikutano ya mawaziri wake wa ulinzi na mambo ya nje na kushirikiana kwa karibu katika sera muhimu. Mkutano huo wa kilele leo utatanguliwa na mkutano wa kibiashara kati ya Ujerumani na Italia.