1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani, nchi zingine zaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani

8 Machi 2026

Ujerumani imejiunga na mataifa mengine duniani kuadhimisha Jumapili (08.03.2026) Siku ya Wanawake Duniani.

Bango linalodai haki sawa kati ya wanawake na wanaume
Bango linalodai haki sawa kati ya wanawake na wanaumePicha: Rahat Dar/dpa/picture alliance

Sherehe na harakati mbalimbali zimeshuhudiwa katika mji mkuu Berlin ambapo watetezi wa haki za wanawake wamelalamikia kuhusu haki na usawa wa kijinsia.

Waziri wa Ujerumani anayehusika na masuala ya Familia, Wanawake na Wazee Karin Prien amesema Ujerumani imepiga hatua katika suala la  usawa kati ya wanawake na wanaume  ambalo amesema ni hitaji la kikatiba, lakini akasisitiza kuwa hali hiyo inaweza kuboreshwa.

Kwa upande wa Afrika, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema maadhimisho ya siku hii yanakumbusha wajibu muhimu kwa vizazi vya sasa na vijavyo wa kuendelea kupanga na kutekeleza mipango ya kumwezesha mwanamke kama juhudi za kukomboa familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW