1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na EU zalaani kunyongwa kwa Jamshid Sharmahd

29 Oktoba 2024

Ujerumani na Umoja wa Ulaya zimelaani vikali hatua ya Iran ya kumnyonga Muirani mwenye pia uraia wa Ujerumani, Jamshid Sharmahd, aliyekuwa na umri wa miaka 69. Sharmahd amenyongwa baada ya kukaa miaka mingi gerezani.

Iran I Jamshid Sharmahd
Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Iran Jamshid SharmahdPicha: fars

Ujerumani na Umoja wa Ulaya zimesema zinatafakari hatua za kulipiza kisasi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kunyongwa Sharmahd ni "kashfa" na Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock ameuonya utawala wa Iran kwamba utajibiwa vikali. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amejibu kupitia mtandao wa kijamii wa X akisema "Pasipoti ya Ujerumani haimfanyi mtu yeyote aepuke adhabu, na hasa mhalifu na gaidi".

Iran yamnyonga Jamshid Sharmahd raia wa Ujerumani na Iran

Ujerumani imewasilisha malalamiko yake kwa Iran. Balozi wa Ujerumani mjini Tehran pia aliwasilisha malalamiko kwa wizara ya mambo ya nje ya Iran na kisha alirudishwa Berlin kwa mashauriano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW