1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ujerumani na Urusi wafukuziana wanadiplomasia

23 Aprili 2023

Urusi imesema itawafukuza zaidi ya wanadiplomasia 20 wa Ujerumani, wakati Berlin ikiarifu baadhi ya wanadiplomasia wa Urusi wameondoka Ujerumani.

Krim l Parlament in Simferopol, Russische Flagge
Picha: Vasily Maximov/AFP via Getty Images

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi, Maria Zarakhova, amesema azma hiyo inafuatia hatua ya Ujerumani ya kuwaondoa watumishi wa ubalozi wake, lakini pia inalenga kupunguza idadi ya wafanyakazi katika ubalozi wa Ujerumani, mjini Moscow.

Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani amesema Berlin na Moscow zimekuwa zikifanya mawasiliano kuhusiana na idadi kamili ya uwakilishi katika wiki chache zilizopita kwa lengo la kupunguza uwepo wa maafisa wa kijasusi wa Urusi nchini humo.

Uhusiano kati ya Urusi na Ujerumani, ambayo ilikuwa mnunuzi mkubwa wa mafuta na gesi ya Urusi, umevurugika tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mapema mwaka uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW