1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Uswisi leo uwanjani

26 Machi 2008

Ujerumani ina miadi leo na Uswisi wakati Uingereza na David Beckham inaumana na Ufaransa huko Paris.

Wakati katika kanda ya Asia, timu kadhaa za taifa zilikuwa uwanjani leo kuania tiketi za kombe lijalo la dunia,huku Ulaya macho yanakodolewa Ufaransa ikiwa na miadi leo na Uingereza wakati Uswisi wenyeji wa kombe lijalo la Ulaya wanaumana na Ujerumani. Brazil,iko London kwa miadi na Sweden.

►◄

Kabla ya Ujerumani kuingia uwanjani jioni hii na uswisi,wenye wa kombe lijalo la Ulaya la mataifa hapo juni 8 na David Bekham akipatiwa nafasi ya kuichezea England mechi yake ya 100 katika timu ya taifa dhidi ya Ufaransa, China ilimudu suluhu tu nyumbani na australia katika kinyan'ganyiro chao cha kuania tiketi za kombe lijalo la dunia nchini Afrika kusini 2010.

Hata ndugu 2 Korea ya kusini na kaskazini ziliachana suluhu leo 0:0.Uzbekistan lakini ilirarua mapande 3 saudi Arabia ilipoichapa mabao 3:0.

Ujerumani ikiongozwa na nahodha wake Michael Ballack inapambana na Uswisi huku langoni akicheza Lehmann-kipa wa Arsenal ambae aliwekewa shaka shaka karibuni.Washambulizi wa Ujerumani Mario Gom,ez wa klabu bingwa Stuttgart na Miros Slav klose,alietia mabao mengi kabisa katika kombe lililopita la dunia.Wachezaji wa kiungo nahodha Ballack na Hitzperger.Upande wa wingi wa kulia na kushoto watatamba akina Schweinsteiger wa Bayern Munich na Schneider wa Bayer Leverkusen.

Kabla mpambano huu,kocha wa Ujerumani Joachim Loew amepitisha kanuni fulani za kufuatwa na wachezaji katika kiu chao cha kutwaa kombe la ulaya mwaka huu.Loew haruhusu wachezaji kutoka usiku sana kwenda madisco na huduma za vyumbani hotelini mwiko.

Hadi hapo bundesliga itakapomaliza msimu hapo mei,wachezaji wa taifa wa ujerumani wanapigwa marufuku kwenda disc katika mkesha mechi za Ligi.Kocha Loew anadai nidhamu katika kipindi hiki kabla ya kombe la ulaya linaloanza Juni 8 nchini uswisi na Austria.

Katika kombe hilo la ulaya, ujerumani imeangukia kundi moja na Poland,Croatia na wenyeji Austria.

Kwa mashabiki wa Uingereza, England ina miadi jioni hii huko Stade de France na jirani zao Ufaransa.Unaweza ukawa usiku wa nahodha wao wa zamani David Beckham kutamba akiichezea leo England kwa mara ya 100 mjini Paris.

David Beckham alivaa jazi ya England kwa mara ya kwanza hapo Septemba mosi, 1996 pale england ilipoikomoa moldova kwa mabao 3:0 katika kinyan'ganyiro cha kuania tiketi za kombe la dunia nchini Ufaransa, 1998.

Beckahm aliichezea Uingereza kwa mara ya 99 dhidi ya croatia uwanjani Wembley ingawa walilazwa mabao 3-2 na kushindwa kukata tiketi ya finali za kombe la ulaya 2008.

Wachezaji 2 wa tim,u ya taifa ya Brazil inayocheza leo na Sweden, wamegonga vichwa vya habari: Mlinzi Lucio hataruhusiwa kuiachamkono Bayern munich kabla mkataba wake kumalizika mwaka 2010,licha ya kuweka matumaini ya kuhamia nchi nyengine kwa dimba.

Mwenyekiti wa bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge ameliambia toleo la leo la gazeti la BILd kwamba, Munich haimudu kumuachia mchezaji mzuri kama Lucio kuiacha mkono.Lucio alijiunga na Munich 2004 kutoka Bayer Leverkusen.Lucio amesema kuwa Ligi za Spain,Itali na Uingereza zinamtamanisha kucheza huko.

Mwenzake Ronaldinho aonesha amechoshwa alao na Ligi ya Spain.Kwani, uhusiano katiyake na klabu yake ya FC Barcelona kwa muujibu wa magazeti ya leo ya Spain umekuwa mbaya na Barcelona huenda ikaachana nae mkono mwishoni mwa msimu huu.Ingawa rais wa barcelona Joan Laporta ameuambia mkutano na waandishi habari jana kwamba ndoa haikuvunjika kati ya barcelona na Ronaldinho, magazeti ya Spain yanavumisha ndoa hiyo imeshavunjwa na swali la ronaldinho kuondoka lilizungumzwa jana katika mkutano wa klabu hiyo.

Nje ya dimba, mwenge wa olimpik utawasili Ufaransa kwa njia ya garimoshi chapa eurostar hapo april 7.Utabakia Ufaransa kwa masaa 24 kabla haukufungishwa safari hadi san Francisco,Marekani.