1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuwarudisha maimamu 1,000 nchini Uturuki

Hawa Bihoga
14 Desemba 2023

Serikali za Ujerumani na Uturuki zimekubaliana juu ya mpango wa kuwarudisha taratibu, maimamu 1,000 wa Kituruki wanaofanya kazi Ujerumani katika miaka michache ijayo.

Deutschland Berlin | Moschee in Wilmersdorf
Picha: Schoening/IMAGO

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imesema Alhamisi kuwa serikali za Ujerumani na Uturuki zimeafikiana juu ya ratiba ya kuwarejesha nyumbani maimamu 1,000 wa Kituruki wanaofanya kazi nchini Ujerumani, katika mamlaka ya Kidini ya Uturuki, Diyanet, katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Kwa miaka mingi wahubiri hao waliotumwa wamezusha utata kwa sababu wahubiri hao, ambao kwa kawaida hutumwa Ujerumani kwa miaka minne, hufuata maagizo kutoka Ankara kama watumishi wa umma wa Uturuki na kwa kawaida hawana ufahamu kamili wa hali halisi ya maisha katika jamii ya Wajerumani.

Maimamu wa Diyanet hufanya kazi hasa katika misikiti inayosimamiwa na shirika la Uturuki la Muungano wa taasisi za dini, Ditib. Kwa mujibu wa serikali ya Ujerumani, dazeni kadhaa miongoni mwao wanahubiri katika mikusanyiko ya Muungano wa vyama vya Utamaduni wa Kiislamu vya Uturuki barani Ulaya, ATIB, na Mili Görüs - taasisi mbili zilizotajwa katika ripoti ya karibuni ya mwaka kutoka idara ya ujasusi wa ndani ya Ujerumani.

Soma pia:Ujerumani inaangazia kusaka suluhu ya uhusiano kati yake na Uturuki ambao mara zote umekuwa mgumu

Ili kupata faida juu ya kinachohubiriwa katika misikiti ya Ujerumani kabla ya mwisho wa kutumwa kwa maimamu, Ditib itabeba jukumu la kitaaluma la wahubiri katika kipindi cha 2024.

Maimamu wapya kupata mafunzo Ujerumani

Serikali ya Ujerumani inataka kuhimiza mafunzo ya ziada ya maimamu nchini Ujerumani. Mafunzo haya ambayo ni wazi kwa wahitimu wa programu zashahada ya theolojia ya Kiislamu, yanapaswa kuwa na nguzo tatu: Masomo ya Kijerumani, elimu ya dini ya Kiislamu na historia ya Ujerumani, masuala ya kijamii na kisiasa na maadili.

Soma pia:Ujerumani yaahidi misaada zaidi kwa Uturuki na Syria

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser alisema:  "Nimefurahi kwamba, baada ya mazungumzo ya muda mrefu, tumeweza kuhitimisha makubaliano na Uturuki kwa mara ya kwanza ambayo yatakomesha utumaji wa maimamu walioajiriwa na serikali kutoka Uturuki."

"Tunataka maimamu wahusishwe katika mazungumzo kati ya dini na kujadili masuala ya imani katika jamii yetu," alisisitiza.

Ujerumani: Rasimu ya kuwarudisha watu katika mataifa yao

01:45

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW