Ujerumani: NATO yapaswa kujiimarisha kufuatia vita Ukraine
3 Oktoba 2023Matangazo
Breuer amesema dalili za kabla ya kunyakuliwa kimabavu kwa Rasi ya Crimea mnamo mwaka 2014 na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwaka jana, hazikuzingatiwa kwa wakati muafaka.
Amesema uvamizi huo haramu unasisitiza umuhimu wa kuwepo vikosi vya jeshi vilivyo tayari kwa mapambano.
Hayo yanajiri wakati Urusi imesema hii leo kuwa haijasitisha majaribio yake ya nyuklia, na imekua mara kadhaa ikiyaonya mataifa ya Magharibi kuwa shambulio lolote dhidi yake linaweza kusababisha majibu ya nyuklia.