1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuUjerumani

Ujerumani: Polisi wakamata tani 2 za madawa ya kokeini

28 Septemba 2024

Polisi nchini Ujerumani wamekamata tani 2 za madawa ya kulevya aina ya kokeini zenye thamani ya dola milioni 112.

Madawa ya kulevya aina ya Kokeine yakiwa yamefichwa kwenye ndizi
Madawa ya kulevya aina ya Kokeine yakiwa yamefichwa kwenye ndiziPicha: UK NATIONAL CRIME AGENCY/AFP

Kokeini hiyo ilifichwa kwenye masanduku ya ndizi yaliyokuwa kwenye kontena huko Rothenburgsort karibu na bandari ya Hamburg. Polisi wamesema hatua hiyo ilitokana na  uchunguzi wa wiki kadhaa.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Hamburg Andy Grote amesema hayo ni mafanikio makubwa katika operesheni ambayo amesema inaendelea. Watu zaidi ya 10 wamekamatwa wakituhumiwa kuhusishwa na tukio hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW