Ujerumani: Sheria mpya ya watumishi wa umma yaanza kutumika
1 Aprili 2024Hatua hizo za kinidhamu zinaweza kuchukuliwa kwa agizo kutoka kwa mamlaka husika na kuwezesha kufutwa kazi kwa watumishi wa umma ama kuondolewa kwa pensheni yao.
Sheria hiyo mpya inapaswa kuisaidia serikali ya nchi hiyo dhidi ya kesi zinazochukuwa muda mrefu mahakamani.
Waziri wa masuala ya ndani asema hawatawavumilia wanaoishambulia serikali kutoka ndani
Sheria hiyo pia inaeleza kuwa kosa la uchochezi wa chuki ambalo kwasasa linabeba adhabu ya kifungo cha hadi miezi sita ama zaidi jela, litasababishia kupotea kwa haki za watumishi wa umma.
Soma pia:Misimamo mikali ya mrengo wa kulia yaongezeka Ujerumani
Siku ya Jumamosi, waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Nancy Faeser, aliwaambia waandishi habari kwamba hawataruhusu taifa hilo la kidemokrasia kushambuliwa kutoka ndani na watu wenye misimamo mikali.