1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

Ujerumani na Somalia kuwafukuza wahamiaji haramu

6 Novemba 2024

Ujerumani na Somalia zitashirikiana katika kuongeza kasi ya kurejeshwa kwa wahamiaji kutoka nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Sheria na Haki | Wahamiaji wakiwa wanahudumiwa.
Afisa uhamiaji akiwa katika majukumu ya kuwahudumia wahamiajiPicha: Rainer Weisflog/IMAGO

Baada ya mkutano na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud mjini Berlin, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema viongozi hao walikubaliana kuwa wahamiaji wasiokuwa na haki ya kisheria kusalia Ujerumani "watarudishwa makwao haraka na kwa ufanisi."

Scholz amesema watakaoathirika zaidi na hatua hiyo ya kufukuzwa ni wahalifu wa makosa makubwa.

Soma pia:Polisi ya Ujerumani yasema idadi ya wanaovuka mpaka yapungua

Kansela huyo ameongeza kuwa uamuzi huo pia ni wa kuyalinda maslahi ya jamii kubwa kabisa ya Wasomali wanoishi Ujerumani na ambao wanaendelea vizuri na wametangamana katika jamii.

Jumla ya Wasomalia 65,000 wanaishi Ujerumani. Kansela Scholz amesema ni idadi ndogo pekee ambao hawana haki ya kuishi nchini humo.