1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani, Ufaransa zatinga 16 bora kombe la dunia

Sylvia Mwehozi
14 Juni 2019

Ujerumani na Ufaransa zimekuwa timu za kwanza kufuzu hatua ya 16 bora baada ya timu hizo mbili kushinda michezo miwili ya kwanza katika mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake linaloendelea Ufaransa. 

Fussball - FIFA Frauen-WM - Deutschland - Spanien
Picha: picture alliance / HMB Media/ Heiko Becker

Mchezaji wa Ufaransa Valerie Gauvin aliipaisha timu yake ambayo ni wenyeji wa mashindano hayo ya kombe la dunia kwa wanawake, mbele ya Norway katika dakika za awali za kipindi cha pili lakini dakika chache baadae walijifunga timu hiyo ilijifunga kupitia kwa Wendie Renard.

Goli la mkwaju lililofungwa na Euginie Le Sommer liliiokoa Ufaransa na kuwapatia tiketi ya hatua ya mtoano wa mashindano hayo bila ya kujali matokeo ya mechi kati yake na Nigeria itakayochezwa Jmatatu. Ushindi wa China dhidi ya Banyana Banyana ya Afrika Kusini uliihakikishia Ujerumani nafasi ya 16 bora siku moja baada ya Ujerumani kupata ushindi dhidi ya Uhispania.

Sara Dabritzy aliipatia Ujerumani goli la pekee katika kipindi cha dakika 42, na kuihakikishia timu yake kuwa kileleni mwa kundi B huku pia akiibuka mchezaji wa mechi.

Rais Infantino wa FIFA na mwenyeji wake rais Macron katika mechi a ufunguziPicha: Imago Images/J. Huebner

Ujerumani siku ya Jumatatu watakutana na Afrika Kusini ambao watakuwa wanakamilisha kampeni katika kinyan'ganyiro hicho cha kombe la dunia kwa Wanawake. Japan ilikuwa ikiongoza dhidi ya Scotlandkatika mchezo wa Ijumaa, huku Jamaica ikiwakaribisha Italia na England dhidi ya Argentina hapo baadae. Kesho wawakilishi wengine wa Afrika Cameroon walioanza vibaya watakwaana na Uholanzi.

Na hapo jana utafiti ulionyesha kuwa zaidi ya mashabiki wa soka milioni 1.5 wanahudhuria mechi za kombe la dunia kwa wanawake linaloendelea nchini Ufaransa na hivyo kuongeza chachu ya umaarufu wa mchezo huo kwa wanawake.

Utafuti huo ulifanywa na Women world Cup in Numbers.com unafuatilia mwenendo na namba katika ukuaji wa kombe la dunia la wanaume na wanawake tangu mwaka 1991, na umebaini kuwa idadi ya watakaohudhuria itafikia mashabiki milioni 1.7 katika jumla ya mechi 52.

Michuano ya Kombe la dunia iliyopita iliyofanyika Canada ilishuhudia watu zaidi ya milioni 1.3 wakitazama michezo ya moja kwa moja. Zaidi ya mashabiki 270,000 walihudhuria siku sita za ufunguzi, na kushuhudia Marekani mabingwa watetezi wakiibugiza Thailand mabao 13-0 na kuweka rekodi.

Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris ulio na uwezo wa kubeba mashabiki 45,000 ulifurika wakati wenyeji walipowashinda Korea Kusini bao 4-0 katika mechi ya ufunguzi wiki iliyopita. Jumla ya magoli 44 yamepachikwa katika mechi 15 zilizokwisha chezwa hadi hivi sasa. dpa/reuters

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW