1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wataka hatua za karantini ziondoshwe Ujerumani

Zainab Aziz Mhariri:Yusuf Saumu
12 Julai 2021

Baada ya kupungua kwa wiki kadhaa, maambukizi ya virusi vya corona yameongezeka tena na kufululiza kwa siku ya tano nchini Ujerumani.Hata hivyo viongozi wanajadiliana juu ya kuondosha hatua zilizobakia za karantini.

Deutschland Coronavirus - Menschen in Restaurants und Bars in Berlin
Picha: Christophe Gateau/dpa/picture alliance

Maafisa wa serikali wanaviondoa vizuizi vya kudhibiti maambukizi ya corona hatua kwa hatua nchini Ujerumani lakini wakati huo huo maambukizi hayo yanaongezeka.

Hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita idadi ya watu walioambukizwa iliendelea kwa siku ya tano mfululizo kwenye sehemu kadhaa za nchi. Licha ya kiwango cha maambukizi kuendelea kuwa cha chini kulinganisha na kipindi cha miezi mitatu iliyopita, viongozi wanaendelea kusisitiza tahadhari hasa kutokana na kuongezeka  haraka kwa maambukizi katika nchi nyingine za Ulaya na pia kutokana na kusuasua kuzirejesha hatua za kuyazuia.

Licha ya hali hiyo baadhi ya viongozi ikiwa pamoja na waliomo kwenye serikali ya kansela Angela Merkel, wanataka vizuizi vilivyobakia vyote viondolewe.

Lothar H. Wieler Mkuu wa Taasisi ya Ujerumani ya kudhibiti maambukizi ya Robert KochPicha: Jens Krick/Flashpic/picture alliance

Taasisi ya Ujerumani, ya Robert Koch ya kuzuia  magonjwa ya kuambukiza imetoa taarifa juu ya watu wengine 745 waliopatwa na covid 19 na pia imeripoti juu ya vifo vingine sita.

Kwa mujibu wa taarifa ya taasisi hiyo imesema idadi ya watu walioambukizwa katika kila laki moja ilioongezeka kwa asilimia 6.2 kwa siku ya tano mfululizo katika muda wa wiki moja. Hata hivyo kiwango cha maambukizi ni cha chini kulinganisha na cha mwezi wa Aprili au mwezi wa Desemba mwaka uliopita ambapo katika kila watu laki moja, zaidi ya 160 walikumbwa na Covid-19.

Taarifa mpya imetolewa wakati ambapo pana wasi wasi unaosababishwa na kuzidi kuenea kwa maambikizi ya virusi vipya aina ya Delta nchini Ureno, Uhispania, Urusi  na Uingereza.

Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens SpahnPicha: CHRISTIAN MANG/REUTERS

Hoja ya kutetea wazo la kuondoa vizuizi vilivobakia, vya kudhibiti maambukizi nchini Ujerumani imepata nguvu kutokana na zoezi la chanjo. Kwa mujibu wa takwimu za idara ya serikali ya kuepusha magonjwa ya kuambukiza asilimia 58 ya watu wanaostahili kupata chanjo wameshapatiwa chanjo ya kwanza nchini Ujerumani na wengine asimilia 42 wameshapatwia chanjo zote kamili.

Wakati huohuo mtaalam wa afya wa Ujerumani Karl Lauterbach amelilaumu Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kwa kushindwa kushughulikia ipasavyo janga la corona wakati wa mashindano ya kombe la Ulaya Euro 2020. Amesema mashindano hayo yalionyesha kana kwamba jangala corona limeisha wakati dunia bado inapambana na watu wanaendelea kupoteza maisha. 

Mashabiki walivyorundikana wakati wa mashindano ya kombe la Ulaya EURO 2020Picha: Christophe Gateau/dpa/picture alliance

Marekani inaongoza ulimwenguni kwa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona na pia kwa vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19 hata hivyo nchi hiyo mpaka sasa imetoa chanjo kwa takriban watu milioni 332 ambayo ni asilimia 55 ya idadi ya watu wa Marekani.

Vyanzo:/DPA/https://p.dw.com/p/3wKAd

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW