1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani watoka sare ya kutofungana na Ukraine

4 Juni 2024

Wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka huu Ujerumani wameanza kupasha misuli moto kwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ukraine usiku wa kuamkia leo, mechi hiyo ikiishia sare ya kutofungana.

Kandanda | Ujerumani ikicheza dhidi ya Ukraine
Timu ya Ujerumani ikicheza dhidi ya UkrainePicha: Daniel Karmann/dpa/picture alliance

Mchezaji wa klabu ya Hoffenheim Maxmilian Beier ndiye aliyepata nafasi za wazi upande wa Ujerumani kwani aligongwa mwamba mara tu baada ya kuingia uwanjani ila juhudi za Ukraine za kujilinda zilizaa matunda na Manuel Neuer akawaokoa pakubwa Ujerumani kutokana na hatari iliyokuwa inaletwa na winga wa Ukraine Mykhaylo Mudryk.

Timu ya taifa ya England ilikuwa inacheza na Bosnia na Herzegovina na ikapata ushindi wa 3-0 Cole Palmer, Trent Alexander Arnold na Harry Kane wakiwa wafungaji wa mabao hayo.

Soma pia:Bayer Leverkusen kuandika historia itakapokutana na Atalanta?

Kwengineko michezoni nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe sasa ni mchezaji rasmi wa mabingwa wapya wa Ulaya Real Madrid.

Hii ni baada ya mshambuliaji huyo kukamilisha uhamisho wake kutoka Paris Saint Germain ambapo kandarasi yake ilikuwa imekwisha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW