1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Watu wahama kutoka mijini kwenda vijijini

Angela Mdungu
27 Septemba 2023

Miji inapanuka na watu wamekuwa wakiyakimbia maeneo ya vijijini kuelekea mijini. Huu ni mtindo ambao umekuwa ukishuhudiwa kwa kiasi kikubwa barani Ulaya kwa miaka mingi.

Mji wa Munich katika mandhari ya kupendeza
Mji wa Munich katika mandhari ya kupendezaPicha: Christian Offenberg/Zoonar/picture alliance

Miji inapanuka na watu wamekuwa wakiyakimbia maeneo ya vijijini kuelekea mijini, huu ni mtindo ambao umekuwa ukishuhudiwa kwa kiasi kikubwa barani Ulaya kwa miaka mingi.

Hata hivyo kwa baadhi ya maeneo ya Ujerumani, hali ni kinyume cha mwenendo huo. 

Wengi husema kuwa maeneo ya vijijini ambako hakuna tena kinachoendelea kuwa yana mfumo dhaifu. Wengi wanaoishi vijijini ni wastaafu.

Huko hakuna tena kazi, hakuna maduka, madaktari wala  idara za zimamoto.

Maeneo mengi ya vijijini kote Ulaya yanakabiliwa na upungufu wa idadi ya watu wakati wengi wao wakivutiwa na miji mikubwa.

Kulingana na mamlaka ya takwimu ya Umoja wa Ulaya ya Eurostat, kati ya mwaka 2015 na 2020, mikoa 355 kati ya 406, mingi ikiwa ni ya vijijini katika Umoja wa Ulaya ilirekodi idadi kubwa ya watu wakihama kuondoka katika maeneo hayo kuliko wale wanaohamia.

Soma pia:Ujerumani yakataa pendekezo la ukomo wa wakimbizi

Idadi ya vijana na watu walio katika umri wa kufanya kazi iliporomoka kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande mwingine, Jumla ya watu wenye miaka 65 na zaidi katika sehemu hizo za vijijini ilipanda kwa wastani wa asilimia 1.8 kwa kila mwaka.

Matokeo yake, miji inazidi kuwa na msogamano na gharama za maisha zinaongezeka.

Pia, kumekuwa na uhaba wa makazi na kumeendelea kuwa na shinikizo la kujenga katika kila eneo lenye kijani.  

Kwa vijijini, nafasi za kazi na hisia za watu kuachwa nyuma kimaendeleo zinazidi kuongezeka.

Hali ya uhamiaji wa ndani Ujerumani

Kwa miongo mitatu, uhamiaji ndani ya Ujerumani ulieleka upande mmoja, kutoka vijijini kwenda mijini.

Muonekano wa mandhari ya mji mdogo Heubach, mashariki mwa Wurttemberg, Ujerumani,Picha: Filip Bubenheimer

Baada ya Ujerumani mashariki na Ujerumani magharibi kuungana mwaka 1990 idadi ya wakaazi katika miji kama vile Leipzig, Munich na Berlin,  wakati mwingine iliongezeka  kwa zaidi ya asilimia 20 kati ya mwaka 2000 na  2020

Hali hii inaonekana kukoma kama ilivyooneshwa na idara ya takwimu ya shirikisho kuanzia mwaka 2008 hadi 2021.

Wakati wanafunzi, watu walio kwenye mafunzo kwa vitendo, na raia wa kigeni wakiendelea kuelekea mijini.

Watu wengi zaidi wenye kati ya miaka 30 na 49 wakiwa na watoto, wataalamu vijana kati ya miaka 25 na 29, wamekuwa wakihamia vijijini tangu mwaka 2017.

Taasisi ya idadi ya watu na maendeleo ya Berlin inayojihusisha na mabadiliko ya kidemografia na matokeo yake imefanya uchambuzi wa takwimu na taarifa kuhusu mabadiliko ya mwenendo wa uhamiaji Ujerumani.

Soma pia:Waziri wa Ulinzi Ujerumani aanza ziara, Mataifa ya Baltic

Imesema kuwa kwa mwaka 2021 karibu theluthi mbili ya jamii za vijijini zimenufaika na uhamiaji.

Katika mahojiano yao, watafiti waligundua kuwa watu wanachokitafuta ni makazi yenyegharama nafuu, mazingira asilia na sehemu zenye kiwango cha chini cha uchafuzi wa mazingira.

Uwezekano wa kufanya kazi kutokea nyumbani kila siku au kwa ujumla, kunamaanisha kuwa watu wengi wako tayari kukubali kuishi mbali na miji.

Utafiti wa taasisi hiyo umeongeza pia kuwa, ulazima wa kuishi karibu na vituo vya hazi haupo tena. Janga la UVIKO 19 lilibadilisha kabisa mwenendo huo. 

Taasisi hiyo ya utafiti wa madiliko ya mwenendo wa kidemografia ya Berlin imebainisha kuwa jambo muhimu kwa wanaohamia vijijini ni uwepo wa miundombinuinayofanya kazipamoja na huduma ya intaneti yenye kasi.

Mji wa Ujerumani ulioachwa wageuzwa makaazi ya wahamiaji

01:45

This browser does not support the video element.