1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
HistoriaUjerumani

Ujerumani yaadhimisha miaka 35 kuangushwa Ukuta wa Berlin

9 Novemba 2024

Ujerumani inaadhimisha leo miaka 35 tangu kuanguka kwa Ukuta wa Berlin tukio lililohitimisha enzi ya utengano na kufungua njia ya kuungana tena kwa iliyokuwa Ujerumani Magharibi na Mashariki.

Ukuta wa Berlin
Ukuta wa Berlin ulitenganisha pande mbili za mji wa Berlin kati ya Ujerumani Magharibi na Mashariki.Picha: Staff Sergeant F. Lee Cockran/Looks Film

Madhimisho ya mwaka huu chini ya kaulimbiu ya "Kuuenzi uhuru" yatafunguliwa na Rais Frank-Walter Steinmeier kwenye eneo la kumbukumbu ya Ukuta wa Berlin. Eneo hilo lilianzishwa kutoa heshima kwa takribani watu 140  waliouawa wakijaribu kuikimbia iliyokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani Mashariki.

Ukuta wa Berlin uliangushwa mnamo Novemba 9 mwaka 1989 na siku hiyo inaadhimishwa nchini Ujerumani kama mwisho wa udikteta wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki na kushindwa na itikadi ya kikomunisti ya Dola ya Kisovieti.

Baadaye leo jioni kutakuwa na onesho la burudani ya muziki na uwashaji wa taa kwenye lango mashuhuri la Brandeburg mjini Berlin, eneo ambako Ukuta wa Berlin ulikatisha na kuzitenganisha pande mbili za mji huo mkuu tangu mwaka 1961.