1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Ujerumani yaagiza kufungwa kwa balozi tatu ndogo za Iran

31 Oktoba 2024

Serikali ya Ujerumani yaamuru kufungwa kwa balozi tatu ndogo za Iran nchini humo katika kujibu hatua ya mauaji ya mfungwa wa Iran mwenye asili ya Kijerumani Jamshid Sharmahd.

Sharmahd, mwenye umri wa miaka 69, aliauwa siku ya Jumatatu kutokana na mashtaka ya ugaidi.
Sharmahd, mwenye umri wa miaka 69, aliauwa siku ya Jumatatu kutokana na mashtaka ya ugaidi.Picha: Koosha Falahi/Mizan/dpa/picture alliance

Sharmahd, mwenye umri wa miaka 69, aliauwa siku ya Jumatatu kutokana na mashtaka ya ugaidi. Haya ni kwa mujibu wa idara ya mahakama ya Iran.

Hatua hiyo inafuatia kesi ya mwaka 2023 ambayo Ujerumani, Marekani na makundi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yaliipuuza na kuiita ya uongo.

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani tayari ilikuwa imemuita afisa mkuu wa kidiplomasia wa balozi hizo ndogo za Iran kulalamika kuhusu mauaji ya Sharmahd.

Balozi wa Ujerumani Markus Potzel, pia alimlalamikia Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, kabla ya kuitwa Berlin kwa mashauriano.

Uamuzi wa kufungwa kwa balozi hizo ndogo mjini Frankfurt, Hamburg na Munich, kulikotangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock  kunaliacha taifa hilo la Kiislamu na ubalozi mmoja tu mjini Berlin.