1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaahidi msaada zaidi wa silaha kwa Ukraine

11 Oktoba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz leo ameahidi msaada zaidi wa silaha kwa Ukraine wa thamani ya dola bilioni 1.5 wakati wa mkutano na rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky mjini Berlin, Ujerumani.

Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky (kushoto) na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (kulia) wakutana mjini Berlin kwa mkutano mnamo Oktoba 11, 2024
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky (kushoto) na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (kulia)Picha: Ebrahim Noroozi/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Wakati wa mkutano na Rais Zelensky, Scholz amesema kuwa msaada huo mpya wa Ujerumani kwa Ukraine, unajumuisha mifumo ya ulinzi wa anga, silaha na droni.

Ujerumani inaendelea kuinga mkono Ukraine

Scholz ameongeza kuwa Ujerumani inaendelea kuiunga mkono Ukraine na kushtumu mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundo mbinu ya kiraia nchini Ukraine ambayo alisema yanalenga kuvunja upinzani wa watu dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Soma pia:Zelensky autangaza 'mpango wa ushindi' Ulaya

Katika mkutano wa pamoja wa viongozi hao wawili na waandishi wa habari huko Berlin Scholz alituma ujumbe wa wazi kwa Rais wa Urusi Vladmir Putin kwamba kutegea kucheleweshwa muda hakutofanikiwa na kwamba hawataacha kuinga mkono Ukraine.

Kwa upande wake, Rais Zelensky alimshukuru kansela huyo wa Ujerumani kwa msaada wa nchi yake dhidi ya Urusi.

Ujerumani imeisaidia zaidi Ukraine kuliko nchini nyingine

Zelensky ameongeza kuwa Ujerumani imeisaidia nchi yake zaidi kuliko nchi nyingine kwa mifumo ya ulinzi wa anga, hali ambayo imeokoa maisha ya maelfu ya raia wa nchi hiyo na pia kutoa ulinzi kwa miji na vijiji vya Ukraine dhidi ya mashambulizi hayo ya Urusi.

Wakati wa mkutano huo mjini Berlin, Zelensky anatarajiwa kumpa Scholz maelezo kuhusu ''mpango wake wa ushindi.''

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani - Papa FrancisPicha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Ziara hii ya Zelensky nchini Ujerumani, inafanyika baada ya kufutiliwa mbali kwa mkutano muhimu wa kilele wa kimataifa katika kambi ya jeshi la Marekani nchini Ujerumani baada ya uamuzi wa Rais wa Marekani Joe Biden wa kubakia nchini mwake kusaidia katika juhudi za kukabiliana na kimbunga Milton.

Zelensky akutana na Papa Francis, Vatican

Mapema leo kabla ya kukutana na Scholz, Zelensky alikutana na Papa Francis huko Vatican ambapo aliomba msaada wa kuhakikisha kurejeshwa kwa watu wazima na watoto waUkrainewaliochukuliwa mateka na Urusi.

Kupitia ujumbe katika mtandao wa X, Rais huyo alisema,''suala la kuwarejesha nyumbani watu wetu kutoka utumwani ndilo lililokuwa lengo langu kuu la kukutana na Papa Francis.''

Kukamatwa na kufukuzwa kwa watu wa Ukraine ni suala chungu

Zelensky pia aliwaambia waandishi wa habari kwamba waandishi, watu mashuhuri, viongozi wa kijamii na watu wa kawaida waliotekwa na Urusi wanapitia mateso katika jela na kambi za nchi hiyo.

Rais huyo ameongeza kuwa kwa watu wote nchini Ukraine, suala na kukamatwa na kufukuzwa kwa watu bado linabaki kuwa chungu mno.

Rais Zelensky alikutana naPapa Francis kama sehemu ya ziara zake katika mataifa ya Ulaya inayolenga kupata usaidizi kutoka kwa washirika wake kabla ya msimu wa baridi kali.

     

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW