1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaandaa mkutano kuhusu Uislamu

Daniel Gakuba
28 Novemba 2018

Mkutano kuhusu Uislamu nchini Ujerumani umefunguliwa leo mjini Berlin, huku wachambuzi wakitarajia mafanikio madogo. Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer mwenye msimamo mkali dhidi ya Uislamu, ndiye mwenyekiti.

Deutsche Islam-Konferenz 2018
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Horst Seehofer akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa mkutano, Ayten KilicarsanPicha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Mhafidhina Horst seehofer, mwanasiasa mwenye msimamo mkali, alisababisha mvutano mwezi Machi alipomkosoa moja kwa moja Kansela Angela Merkel akiipinga kauli yake kwamba "Uislamu una nafasi  yake Ujerumani." Waziri mkuu huyo wa zamani wa mkoa wa Bavaria alisema Waislamu wanaoishi hapa bila ya shaka ni sehemu ya Ujerumani, lakini haimaanishi kwamba Wajerumani asilia wanaacha utamaduni na mila zao kwa kile alichokiita zingatio lisilo na ukweli, alisisitiza Seehofer wakati wa mahojiano na gazeti la Bild.

Katika mkutano wa mwaka huu kuhusu Uislamu Ujerumani, Seehofer amefanya mabadiliko, akiwaalika  wanazuoni wa elimu ya  dini wenye msimamo wa wastani pamoja na wanasayansi, mbali na Jumuiya za Kiislamu nchini Ujerumani. Mkutano huo unawakusanya pamoja waislamu wa Ujerumani na  wawakilishi wa serikali ya Shirikisho , mikoa na serikali za mitaa. Mwaka huu Seehofer anatarajiwa kulizingatia suala la  ushawishi wa kigeni kwa misikiti na jamii  ya Waislamu nchini Ujerumani na hasa  ushawishi wa Uturuki.

Mkono wa Uturuki katika Uislamu nchini Ujerumani

Uturuki ni mdau muhimu katika Jumuiya ya Waislamu nchini UjerumaniPicha: picture alliance/dpa/C. Soeder

Chama cha  Waislamu kwa  ajili ya taasisi ya  dini  cha waturuki DITIB ambayo ni Jumuiya kubwa kabisa  ya Kiislamu nchini Ujerumani, kinadhibitiwa na Uturuki kupitia  Idara ya  masuala ya dini (Diyanet) mjini Ankara, ambayo huwalipa  mishahara maimamu wa kiasi ya misikiti 900 nchini Ujerumani. Jumuiya ya  DITIB inakosolewa kwa kuwa karibu  na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ambaye wapinzani wake wa nje na ndani wanamuangalia kama anayeiongoza nchi yake kiimla.

Kabla ya mkutano huo  mjini Berlin,  Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani limetoa wito kutaka paweko na  imani na shughuli zinazofanywa na misikiti. Katika mahojiano na kundi la  wachapishaji linalojiita mtandao wa wahariri, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Ujerumani, Aiman Mazyek, alionya dhidi ya kuichukulia misikiti kuwa tatizo, akiongeza kwamba kinyume chake misikiti ni suluhisho. pamoja na hayo aliungama kwamba kuna mapungufu katika jamii za Waislamu.

Chama cha upinzani cha Kijani "Die Grüne" kimeelezea wasiwasi wake juu ya Waziriv wa ndani seehiofer kuwa mwenyekiti wa mkutano huo, huko Kiongoziv wa wabunge wa chama hicho katika bunge la shirikisho Bundestag Katrin Goering-eckard  akiliambia Shirika la habari la Ujerumani DPA, kwamba muda mwingi unaotumiwa kwa mjadala, ungepaswa kwanza kutumika  katika kuweka mazingira bora, badala ya kusababisha matatizo.

 

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman

Mhariri: Mohamed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW