Chini ya uongozi wa Kansela Angela Merkel, Ujerumani itashikilia wadhifa huo kwa muda wa miezi sita. Ujerumani itakuwa na jukumu la kuandaa na kusimamia mikutano baina ya wakuu wa serikali wa Umoja wa Ulaya na mawaziri, chini ya kauli mbiu ya “Pamoja kwa mustakabli wa Ulaya.”