1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yafikia lengo la NATO kutenga fedha za kujilinda

Hawa Bihoga
15 Februari 2024

Ujerumani imefikia lengo la Jumuiya ya Kujihami ya mataifa ya Magharibi NATO la nchi wanachama kutumia 2% ya pato la ndani kwa ajili ya masuala ya ulinzi, huku matumizi hayo yakiongezeka baada ya vita vya Urusi, Ukraine.

NATO, Ubelgiji | Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO Jens StoltenbergPicha: Dursun Aydemir/Anadolu/picture alliance

Serikali ya Ujerumani kwa mwaka huu ulitenga sawa na dola bilioni 73.41 kwa ajili ya matumizi kwenye sekta ya ulinzi, kwa rekodi za Ujerumani hii itakuwa ni sawa na asilimia 2.01 ya pato lake la ndani. Wizara ya Ulinzi Ujerumani haijazungumza chochote kuhusiana na kufikiwa kwa lengo hilo.

Itakumbukwa kuwa mapema wiki hii Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema kuwa Ujerumani itafikia malengo ya Jumuiya ya Kujihami NATO, lakini hata hivyo hadi sasa serikali haijatoa takwimu zozote.

Serikali ya Kansela Scholz imeangazia kuongezeka kwa matumizi yake katika sekta ya ulinzikatika wakati usio na uhakika. Mwishoni mwa juma lililopita Rais wa zamani wa Marekani ambaye ameonesha nia ya kuwania Urais katika uchaguzi ujao Donald Trump alisema kuwa hatawalinda nchi wananchama wa NATO ambao hawatumii fedha za kutosha katika sekta yake ya ulinzi.

Soma pia:Scholz: Kauli ya Trump kuhusu NATO ni ya kutowajibika na hatari

Akijibu hoja hiyo katika mahojiano kwenye kituo cha runinga cha WELT Jumanne jioni, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius alisema Trump alihatarisha kuharibu uhusiano kati ya Ulaya na Marekani.

Pistorius kadhalika hakukubaliana na mapendekezo ya upinzani kwamba Ujerumani inapaswa kuongeza hazina yake maalum ya kijeshi hadi euro bilioni 300 kutoka bilioni 100, akisema kuwa serikali inapaswa kuzingatia bajeti yake katika matumizi ya kawaida pia.

Aidha Waziri huyo wa ulinzi hakukubaliana na hoja ambayo ilizusha mjadala mkubwa baada ya matamshi ya Donald Trump, ya kuundwa kwa muungano tofauti wa ulinzi wa masuala ya nyuklia Ulaya.

"Ninaonya dhidi ya kuanzisha mjadala kama huo, sababu Donald Trump anaetoa matamshi hayo sio hata mgombea urais." Alisema Pistorius.

Wanachama 18 kufikia lengo la NATO- 2024

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema leo Jumatano kuwa, nchi kumi na nane kati ya thelathini na moja za NATO zitafikia lengo la kutenga asilimia mbili kutoka katika mapato yao ya ndani kwa ajili ya masuala ya ulinzi mnamo 2024.

Mkutano Mkuu wa NATOPicha: NATO/IMS

Katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Brussels nchini Ubelgiji Stoltenberg aliongeza kuwa, matumizi jumla ya kijeshi yamewekwa katika mwaka mwingi?, wakati vita kamili vya Urusi nchini Ukraine vikianza mwaka wake watatu.

"Mataifa ya NATO ya Ulaya kwa mwaka huu yatawekeza jumla ya dola bilioni 380 katika masuala ya ulinzi kwa mwaka huu." Alisema Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi NATO

Soma pia:Mkutano wa Scholz na Biden, kipi kitarajiwe?

Ujerumani itafikia lengo la asilimia mbili mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita baridi. Mnamo mwaka 2023, washirika kumi na moja walitarajiwa kufikia lengo la 2% kulingana na makadirio ya awali ya NATO, ambao ni Poland, Marekani, Ugiriki, Estonia, Lithuania, Finland, Romania, Hungary, Latvia, Uingereza na Slovakia.

Takwimu hizo mpya zinatolewa siku chache baada ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kupendekeza kwamba Marekani huendaisiwalinde washirika wa NATO ambao hawatumii fedha za kutosha kujilinda kutokana na kitisho cha uvamizi unaowezekana wa Urusi.

Ujerumani: Hatutaiacha Ukraine kwenye vita peke yake

02:23

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW