1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Ujerumani yahimiza juhudi za upatanishi Niger

4 Agosti 2023

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imehimiza kuendelea kwa juhudi za upatanishi nchini Niger.

Nigeria Abuja | ECOWAS-Treffen zur Lage in Niger
Picha: KOLA SULAIMON/AFP

Baada ya ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS kuondoka patupu mjini Niamey na kushindwa kuirejesha madarakani serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Soma pia: Niger yavunja makubaliano ya kijeshi na Ufaransa

Urusi imesema hii leo kuwa uingiliaji wowote kutoka mamlaka zisizo za kikanda kama vile Marekani, hautotatua mzozo wa Niger. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema Urusi inafuatilia kwa karibu hali hiyo na ina wasiwasi kuhusu mvutano unaoendelea katika eneo hilo.

Rais Mohamed Bazoum aliyepinduliwa madarakani ameitolea wito Marekani na Jumuiya ya kimataifa kusaidia kurejesha utulivu wa kikatiba. ECOWAS  ambayo imewawekea vikwazo viongozi wa kijeshi imetishia uwezekano wa kuingilia kati kijeshi iwapo kufikia Jumapili hii, rais Bazoum hatorejeshwa madarakani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW