1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaiomba radhi Tanzania kwa makosa ya ukoloni

1 Novemba 2023

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesikitishwa na kile alichokiita aibu ya makosa yaliyofanywa wakati wa ukoloni wa Ujerumani nchini Tanzania na kuahidi kutoa ufahamu wa ukatili uliotokea.

Bundespräsident Steinmeier in Tansania
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier akiweka shada la maua katika makumbusho ya vita vya maji maji huko Songea TanzaniaPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesikitishwa na kile alichokiita aibu ya makosa yaliyofanywa wakati wa ukoloni wa Ujerumani nchini Tanzania na kuahidi kutoa ufahamu wa ukatili uliotokea atakaporejea Ujerumani.

Alipokuwa ziarani katika makumbusho ya Maji Maji yalioko katika mji wa Kusini wa Songea, rais huyo wa Ujerumani aliliomba radhi taifa hilo kwa maovu yaliyotokea wakati huo.

Steinmeier ametamka kwamba "ningelipenda kuomba msamaha kwa kile Wajerumani walichofanya kwa wazee wenu hapa, kilichotokea hapa ni historia yetu ya pamoja.  Nataka kuwahakikishia kuwa Wajerumani watakuwa nanyi kutafuta majibu ya masuali ambayo hayajajibiwa yanayowakosesha amani".

Tanzania ilikuwa sehemu ya Ujerumani ya Afrika Mashariki iliyopitia moja ya kipindi kibaya cha umwagikaji wa damu katika enzi za ukoloni kati ya mwaka 1905 hadi 1907. Watalamu wamesema kati ya watu laki mbili hadi laki tatu waliuwawa wakati wa vita vya majimaji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW