1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Ujerumani yamfumkuza balozi wa Chad

11 Aprili 2023

Ujerumani imeamuamuru Balozi wa Chad mjini Berlin kuondoka ndani ya kipindi cha masaa 48 kujibu hatua kama hiyo iliyochukuliwa na taifa hilo la Afrika ya Kati wiki iliyopita.

Mariam Ali Moussa
Picha: Dean Calma/IAEA/Wikipedia

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani, Balozi Mariam Ali Moussa, anapaswa kuondoka haraka.

Vyanzo viwili kutoka serikali ya Chad vilisema siku ya Jumamosi kwamba Balozi wa Ujerumani nchini humo,  Gordon Kricke, alifukuzwa kutokana na kauli zake  tete juu ya hali ya kisiasa nchini Chad.

Hata hivyo, wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani imekanusha balozi wake huyo kutenda kosa lolote lile, na badala yake imesema Balozi Kricke alikuwa akitekeleza majukumu yake ipasavyo akiwa ameshiriki kwenye mazungumzo juu ya haki za binaadamu na kurejea haraka kwa utawala wa kiraia nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW