1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yamfuta kazi Kocha Hansi Flick

11 Septemba 2023

Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) limemfuta kazi kocha wa timu ya taifa ya kandanda Hansi Flick, siku moja baada ya Ujerumani kuchapwa mabao 4-1 na Japan mjini Wolfsburg.

Bundestrainer Hans-Dieter Flick
Picha: Pressefoto Baumann/imago images

Flick ambaye alishikilia wadhifa huo kwa miaka miwili amekuwa na msururu wa matokeo duni.

Gazeti la Bild limesema kocha wa zamani wa  Bayern Munich  Julian Nagelsmann ndiye anatazamiwa zaidi kuchukua nafasi hiyo.

Uamuzi wa kumtimua Flick unajiri ikiwa imesalia miezi 9 kabla ya kuanza michuano ya kuwania kombe la Ulaya hapa nchini Ujerumani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW