1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yamuita balozi wa Iran

16 Januari 2023

Balozi wa Iran nchini Ujerumani ameitwa kuhojiwa kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha wiki moja na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock kuhusiana na wimbi la kunyongwa watu kadhaa na serikali ya Iran.

Deutschland | Demonstration in Hamburg gegen Regime im Iran
Picha: Georg Wendt/dpapicture alliance/dpa

Msemaji wa waziri Annalena Baerbock, Christopher Burger amethibitisha kuhusu hatua hiyo baada ya kuulizwa kuhusu kuhojiwa kwa balozi Mahmoud Farrazandeh. Nchi mbali mbali za Magharibi na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu wamelaani ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Iran kufuatia kunyongwa kwa watu kadhaa waliokuwa wakizuiliwa jela. Jumamosi Iran ilisema imemnyonga raia wake mmoja mwenye uraia pia wa Uingereza aliyehukumiwa kifo kwa kuendesha ujasusi nchini Iran kwa niaba ya Uingereza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW