1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaondoshwa kombe la dunia Urusi

Sylvia Mwehozi
28 Juni 2018

Ujerumani, waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe la dunia na washindi mara nne wa michuano hiyo, wameondolewa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1938 baada ya kuchapwa na Korea Kusini mabao 2-0.

FIFA Fußball-WM 2018 in Russland | Deutschland verliert gegen Südkorea - Enttäuschung - Gomez und Hummels
Picha: Reuters/M. Dalder

Ujerumani, waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe la dunia na washindi mara nne wa michuano hiyo, wameondolewa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1938 baada ya kuchapwa na Korea Kusini.

Magoli ya dakika za lala salama kutoka kwa Korea Kusini, yalilizamisha jahazi la Ujerumani, ambalo tangu mwanzo lilionekana kuyumba baada ya kutandikwa na Mexico katika mechi yake ya ufunguzi.

Tayarin kocha wa kikosi hicho Die Mannschaft Joachim Löw yupo katika shinikizo la kujiuzulu.

Licha ya matokeo hayo, timu zote mbili Korea Kusini na Ujerumani zimefungasha virago na kuipatia nafasi Sweden na Mexico kuelekea hatua ya mchujo.

Timu pekee iliyosalia kutoka Afrika ya Senegal itakuwa na kibarua kizito, baadae hii leo pale itakapokwaana na Colombia katika mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi kuelekea hatua ya mchujo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW