Ujerumani yaongeza msaada wake kwa Pakistan
15 Agosti 2010Matangazo
Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Dirk Niebel amesema msaada wa haraka kutoka jumuiya ya kimataifa ni jambo muhimu ili kuwazuia Waislamu wenye itikadi kali pamoja na kundi la Taliban kusambaza ushawishi wao miongoni mwa watu wanaoteseka nchini Pakistan.
Waziri Mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani ameiomba jumuiya ya kimataifa msaada zaidi akisema kuwa mafuriko hayo yameharibu akiba ya chakula pamoja na mazao.
Wakati huo huo watu kiasi ya millioni 20 wameathiriwa na mafuriko hayo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon hii leo anatarajiwa kutembelea maeneo yaliyokumbwa na janga hilo.
Mwandishi:Aboubakary Liongo
Mhariri:Prema Martin