Ujerumani yaonya kupanuka kwa mgogoro Mashariki ya Kati
18 Machi 2026
Matangazo
Wadephul amesema 'mashambulizi yasiyo ya msingi kabisa, yanayoyalenga mataifa ya Ghuba kwa sasa pia yanaonyesha kwamba kuna uwezekano wa vita kuongezeka.
''hali inaweza kulitumbukiza sio eneo hili la Mashariki ya Kati bali ulimwengu mzima unaweza kutumbukia katika mgogoro mkubwa na mbaya zaidi.''
Wadephul ameongeza kusema kuwa lazima wajaribu kutafuta namna ambayo malengo ya kijeshi ya Marekani na Israel yanaweza kufikiwa ili kupunguza mapigano na kukomesha uhasama.
Akiwa pamoja na Wadephul mjini Berlin, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot pia alitoa wito wa kusitishwa haraka kwa vita na kukomeshwa kwa uhasama.