Ujerumani yapeleka mitambo ya kusafisha maji Pakistan
27 Agosti 2010Matangazo
Wasaidizi hao watawapatia wahanga wa mafuriko nchini Pakistan, maji safi ya kunywa.Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere mjini Berlin alisema kuwa mitambo hiyo inaweza kusafisha lita 12,000 za maji kwa saa na itawekwa katika wilaya ya Punjab iliyoathirika vibaya.
Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa mwito katika televisheni ya Ujerumani kuhimiza michango ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko nchini Pakistan.Hadi sasa,serikali ya Ujerumani imeahidi kutoa msaada wa Euro milioni 25.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hivi sasa nchini Pakistan,kiasi ya watu milioni tatu na nusu hawana maji safi ya kunywa.
Mwandishi: P.Martin/ZPR