1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Mpango wa amani Ukraine ujadiliwe kwa kina

21 Novemba 2025

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Johann Wadephul amesema anauona mpango unaungwa mkono na Marekani wa kumaliza vita Ukraine, una mambo mengi ya kujadiliwa kwa haraka kati ya Urusi na Ukraine.

Johann Wadephul Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani
Ujerumani yasema mpango wa amani ya Ukraine unahitaji kujadiliwa kwa haraka na pande hasimuPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa mpango huo sio wa mwisho.

Akizungumza katika mkutano  wa Indo-Pasifiki, mjini Brussels Wadephul amesema msimamo wa Ujerumani ni sawa na msimamo wa Ulaya ambao unaiunga mkono kikamilifu Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

"Na ni lazima iwe wazi kabisa, kwamba Ukraine inaweza kudumisha uhuru wake katika eneo lake lote.  Lazima kuwa na majadiliano yaliyo na masharti sawa, na hiyo sio tu muhimu kwa Ukraine lakini ni kumhimu pia kwa ulaya. Kwasababu sote tunaona kuwa Urusi inajihami kwa hali ambayo Ulaya ina haki ya kuuliza hili linamfaidi nani," alisema waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani.

Mpango huo unaitaka Ukraine kupunguza nusu ya ukubwa wa jeshi lake na kuachilia majimbo ya mashariki yanayokaliwa na Urusi ikiwa ni pamoja na Donetsk na Luhansk.

Kwa upande wake Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema umoja huo utaunga mkono mpango wowote wa amani ya Ukraine ilimradi ulete amani ya kudumu katika taifa hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW