1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu uachane na matumizi ya makaa ya mawe na mafuta

5 Desemba 2023

Ujerumani inayashinikiza mataifa yanayoshiriki mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi wa COP28 kukubaliana na mpango wa kimataifa wa kuondokana kabisa na matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi.

Regierungskonsultationen Deutschland Brasilien | Olaf Scholz trifft Luiz Inacio Lula
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Wajumbe kwenye mkutano huo wameeleza kwamba Ujerumani imekabiliwa na upinzani wa serikali nyingi kati ya 200 zinazoshiriki mkutano huo wa kilele mjini Dubai. Mjumbe maalum wa Ujerumani katika mkutano huo Jennifer Morgan amesema lengo kuu la nchi yake liko wazi na ambalo ni kuunga mkono nishati mbadala.Waziri wa nishati wa Saudi Arabia, AbdulAziz bin Salman ni miongoni mwa wanaopinga kabisa mpango huo wa pamoja wa makubaliano ya kuondokana na  nishati ya makaa ya mawe,mafuta na gesi. Amezishutumu nchi zinazoshinikiza mpango huo wa kuondokana na matumizi ya nishati ya visukuku  kuwa na undumilakuwili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW