Ujerumani yataka uingiliaji wa mataifa ya kigeni Libya ukome
28 Oktoba 2019Matangazo
Waziri huyo amesema uingiliaji huo, alioutaja kuwa ''tatizo la kimsingi'' kwa Libya, utakuwa mada muhimu katika mkutano utakaofanyika baadaye mwaka huu mjini Berlin kwa ajili ya Libya.
Maas ameyasema hayo jana jioni (27 Oktoba) katika mkutano na waandishi wa habari, akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, Mohamed Siala, na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Ghassan Salame, katika mji wa Zuwara ulioko magharibi mwa Libya.
Tangu mwezi Aprili mwaka huu, Libya imekuwa ikishuhudia kuibuka kwa uhasama mpya, kufuatia mashambulizi ya vikosi vinavyoongozwa na mbabe wa kivita, Khalifa Haftar, dhidi ya serikali ya mjini Tripoli.