1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatangaza kikosi cha kombe la Mashirikisho

17 Mei 2017

Sandro Wagner ni miongoni mwa wachezaji wapya walioteuliwa na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew Jumatano, katika kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki kombe la mashirikisho litakaloandaliwa nchini Urusi.

Fußball Nationalmannschaft Löw bei DFB-Pk in Frankfurt
Joachim Loew wakati wa kukitaja kikosi cha timu ya taifa ya UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa/A. Dedert

Loew atawapumzisha wachezaji wake nyota Sami Khedira, Mesut Oezil, Toni Kroos, Mats Hummels, Thomas Müller na Jerome Boateng kwa kipute hicho kitakachochezwa kati ya tarehe 17 Juni na Julai 2.

Wachezaji wengine nyota kama nahodha na mlinda lango nambari moja Manuel Neuer, Mario Goetze, Benedikt Howedes na IIkay Gundogan wana majeraha, ila Marco Reus na Mario Gomez hawakuchaguliwa naye mshambuliaji Max Kruse hakuitwa tena kikosini.

Kikosi hicho ambacho kitashiriki mechi ya kirafiki Juni 6 dhidi ya Denmark na kicheze mechi ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya San Marino siku nne baadae, kina wachezaji watatu pekeyake walioshinda kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil, Julian Draxler, Matthias Ginter na Shkodran Mustafi.

Wagner anayeichezea Hoffenheim na mwenye umri wa miaka 29, atakuwa anaichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza pamoja na mchezaji mwenzake wa Hoffenheim Karim Demirbay, Lars Stindl wa Borussia Moenchengladbach, Marvin Plattenhardt wa Hertha Berlin, Amin Younes wa Ajax Amsterdam ya Uholanzi na Diego Demme anayeichezea RB Leipzig.

"Sandro Wagner analeta ladha maalum katika timu. Amefunga magoli mengi katika Bundesliga katika miaka miwili iliyopita," Loew aliwaambia wanahabari.

Mshambuliaji wa Hoffenheim Sandro Wagner ameitwa kikosini kwa mara ya kwanzaPicha: picture-alliance/dpa/P. Steffen

Kikosi hicho cha Loew kitakutana tarehe 4 ya mwezi Juni kwa kile kocha huyo alichokiita msimu wa majira ya joto ulio na changamoto maalum. Lakini amepuuza tetesi kwamba timu yake haitatoa ushindani kama ilivyokuwa katika mashindano yaliyopita kutokana na kuwa kwa sasa inaonekana dhaifu.

Kikosi kamili:

Walinda lango: Bernd Leno (Bayer Leverkusen), Marc-Andre ter Stegen

(Barcelona), Kevin Trapp (Paris Saint-Germain)

Mabeki: Matthias Ginter (Borussia Dortmund), Jonas Hector

(Cologne), Benjamin Henrichs (Bayer Leverkusen), Joshua Kimmich

(Bayern Munich), Shkodran Mustafi (Arsenal), Marvin Plattenhardt

(Hertha Berlin), Antonio Ruediger (Roma), Niklas Suele (Hoffenheim)

Viungo/Washambuliaji: Julian Brandt (Bayer Leverkusen), Emre Can

(Liverpool), Julian Draxler (Paris Saint-Germain), Leon Goretzka

(Schalke), Sebastian Rudy (Hoffenheim), Leroy Sane (Manchester City),

Sandro Wagner (Hoffenheim), Lars Stindl (Borussia Moenchengladbach),

Kerem Demirbay (Hoffenheim), Amin Younes (Ajax), Diego Demme

(RB Leipzig), Timo Werner (RB Leipzig)

Mwandishi: Jacob Safari/DPA

Mhariri: Sekione Kitojo

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW