1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatoa Euro 29 milioni EAC

Veronica Natalis
6 Julai 2022

Ujerumani imetoa kiasi cha Euro 29 milioni kwa jumuiya ya Afrika Mashariki, ili kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, katika sekta ya elimu,mazingira na dijitali, fedha ambazo zitanufaisha nchi wanachama zote saba,

Deutschland Tansania Vertragsunterzeichnung in Arusha
Picha: Deutsche Botschaft,Tansania

Miongoni mwa miradi ambayo fedha hizo zitaelekezwa nipamoja na sekta ya kidijitali katika masuala ya ujuzi, uhifadhi wa maliasili hasa maji pamoja na miradi ya  kuhimili athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Fedha hizo zitagawanywa kwa nchi zote saba za jumuia hiyo kongwe barani Afrikana ambazo zimekuwa zikijikwamua katika changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Katika hafla ya utiaji saini mkataba huo ambayo imefanyika katika makao makuu ya jumuia hiyo mjini Arusha Kaskazini mwa Tanzania ujumbe wa Ujerumani umeahidi kushirikiana vilivyo na jumuia hiyo.

Mkuu wa ujumbe wa Ujerumani Claudia Imwode Kraemer kutoka wizara ya Ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo ya shirikisho la Ujerumani alibainisha kuwa makubaliano baina ya Ujerumani na EAC katika kufadhili miradi hiyo ndani ya siku moja.

"Mazungumzo zaidi katika miezi ijayo, yatatupa mwelekeo ni kwa jinsi gani Euro milioni 10 zitatumika, kwaajili ya kuimarisha miundombinu." Alisema Kraemer baada ya zoezi la utiaji saini.

Soma Pia:Wakuu wa Afrika Mashariki wakubali kupeleka jeshi, DRC

Alioneza kuwa "miongoni mwetu hapa tutapata nafasi ya kutembelea kamisheni ya bonde la ziwa Viktoria Kisumu nchini Kenya."

Aidha alitoa wito pia kwa jumuiya ya Afrika Mahsariki kutafuta suluhu ya mgogoro unaendelea Mahsariki mwa Congo ili raia wake ambao kwa sasa ni wanachama wa jumuiya wanufaike na nchi yao.

EAC yaweka bayana mgawanyiko wa fedha hizo

Pesa hizo zitatumika kuendeleza miradi inayohusu elimu na mafunzo, uhifadhi wa Maliasili hasa maji katika bonde la ziwa Victoria na , ufadhili wa masomo kupitia benki ya maendeleo ya Ujerumani KfW, pamoja na ufadhili wa masomo kwa ngazi ya shahada ya uzamili kwa wanafunzi wasiojiweza kiuchumi.

Wakuu wa nchi wa EAC wakiwa katika mkutano kwa njia ya dijitaliPicha: Philbert Rweyemamu/EAC

Katika pesa hizo, kiasi cha Euro milioni 2.5 zimetengwa kwaajili ya kutekeleza mradi kidijitali kwa sekta bunifu Afrika Mahsariki, unaosimamiwa na shirika la misaada la Ujerumani GIZ kupitia mradi wa dskills@EA unaotekelezwa kwa kushirikiana na chou kikuu cha sayansi na teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Arusha Tanzania.

Soma PiaViongozi wa EAC wakutana kujadili usalama wa Kongo

Dr. Peter Mathuki ni katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mahsariki,mabadiliko ya tabia nchi imekuwa ni changamoto kwa dunia nzima, Afrika mashariki nayo imeathiriwa pakubwa hivyo fedha hizo zitakwenda kusaidia pia upande wa mazingira.

Kumekuwa na ushirikiano wa kimaendeleo wa muda mrefu baina ya Ujerumani najumuiya ya Afrika Mashariki, na ushirikiano zaidi utazamiwa katika siku zijazo. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW