1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yahimiza kufanyika juhudi kuzuia migogoro

29 Julai 2024

Ujerumani imezitolea mwito pande zote katika mgogoro wa mashariki ya kati hasa Iran kuchukua hatua kuzuia kutanuka kwa mgogoro huo baada ya shambulio la roketi kuuwa watoto na vijana 12 katika eneo la milima ya Golan.

Waziri wa mambo ya nje ya Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa mambo ya nje ya Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Annette Riedl/dpa/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani amesema  shambulio hilo linaloaminika kufanywa na kundi la Hezbollah pamoja na vitendo vya hivi karibuni vya wanamgambo wa Kihouthi wa Yemen  yamechangia hali mbaya ya uthabiti katika eneo hilo.

Makundi ya Hezbollah na Wahouthi yote wanaungwa mkono na Iran.

Soma pia: Baerbock afanya ziara Ivory Coast baada ya Senegal 

Kwa mujibu wa msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani waziri Annalena Baerbock amefanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa Lebanon ikiwemo waziri mwenzake wa mambo ya nje kujaribu kuzuia kutanuka kwa mgogoro huo.

Ujerumani pia imewashauri raia wake takriban 1,300 walioko Lebanon waondoke wakati huu ambapo bado hali inaruhusu.