1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kufanya mazungumzo na mamlaka mpya ya Syria

17 Desemba 2024

Ujerumani inapanga kuandaa mazungumzo na wawakilishi wa kundi la waasi wa Syria la Hayat Tahrir al Sham, HTS, mjini Damascus.

Deutschland Berlin 2024 | Kanzler Scholz Vertrauensabstimmung im Bundestag
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akitoa hotuba yake siku ya kura ya imani iliyoitishwa na yeye mjini Berlin, Ujerumani, Desemba 16, 2024.Picha: Lisi Niesner/REUTERS

Ikiungana na Marekani pamoja na Uingereza katika harakati za kuwa na mawasiliano na kundi hilo baada ya kuuangusha utawala wa Bashar Al Assad. Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema mazungumzo ya Ujerumani na wawakilishi wa kundi hilo yatazingatia kipindi cha mpito kwa Syria na ulinzi wa makundi ya wachache. Mgogoro wa Syria ulioanza mwaka 2011 ulisababisha wakimbizi zaidi ya milioni moja kukimbilia Ujerumani. Na kuanguka kwa Utawala wa Assad kumezua gumzo nchini Ujerumani kuhusu mchakato wa waomba hifadhi kutoka Syria uliositishwa kwa sasa ili kufuatilia hali nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW