1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaupiga marufuku mtandao wa Samidoun

3 Novemba 2023

Serikali ya Ujerumani imeupiga marufuku mtandao wa uetetezi wa wafungwa wa Kipalestina, Samidoun, na kutangaza hatua zaidi za kuondoa kabisaa uugwaji mkono wa kundi la Hamas

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser 
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser Picha: MICHELE TANTUSSI/AFP

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser  amesema Samidoun, kama mtandao wa kimataifa, unaeneza propaganda dhidi ya Waisraeli na Wayahudi chini ya kisingiziyo cha shirika la kusimamia mshikamano wa wafungwa katika mataifa tofauti.

Wizara hiyo imesema kama matokeo ya marufuku hiyo, mali zozote za kundi hilo zitachukuliwa, na uwepo wowote wa mtandaoni au shughuli za mitandao ya kijamii za kundi hilo zitaharamishwa.

MSF: Majeruhi zaidi ya 20,000 bado wamekwama Gaza

Yeyote anayeendelea kuendesha shughuli kwa ajili ya mashirika hayo anatenda kosa la jinai, imesema wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani.

Awali Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alikuwa ameshatangaza kwamba Ujerumani, inapiga marufuku shughuli za mashirika mawili, muda mfupi baada ya Hamas kuishambulia Israel Oktoba 7.

Watu  takriban 450 wanakisiwa kuliunga mkono Hamas

Waandamanaji mjini Berlin wanaopinga mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Shirika la upelelezi wa ndani nchini Ujerumani  BfV  linakadiria kuwa watu takriban 450 nchini humo wanaliunga mkono Kundi la Hamas ambalo tayari limeorodheshwa kama kundi la kigaidi barani Ulaya. Makundi yaliyo na mafungamano na kundi hilo pia yamepigwa marufuku kwa miaka mingi sasa Ujerumani.

Tathimini ya  BfV inasema mtandao wa Samidoun unaonyesha chuki ya wazi wazi dhidi ya Israel na una mafungamano ya moja kwa moja na vuguvugu la kizalendo la ukombozi wa Wapalestina, PFLP, linalotoa wito wa mapambano ya silaha dhidi ya Israel.

Majeshi ya Israel yakaribia kuingia Gaza City

Kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani, Samidoun pia inaendesha operesheni zake Ujerumani ikitumia jina la HIRAK au "Vuguvugu la Uhamasishaji wa Vijana wa Kipalestina."

Wizara hiyo inaishtumu Samidoun na makundi washirika wake kwa kufanya kazi kudhoofisha mshikamano wa amani wa makundi tofauti ya Ujerumani na imelielezea kama tishio kwa amani ya umma kutokana na uungaji wake mkono matumizi ya vurugu.

Mtanziko wa Ujerumani juu ya azimio la Umoja wa Mataifa

03:02

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW