Ujerumani yawakutanisha viongozi wa Armenia, Azerbaijan
28 Februari 2024Ujerumani inaongoza juhudi za upatanisho kati ya Azerbaijan na Armenia, ikiwa mwenyeji wa mazungumzo hayo ya amani chini ya wizara yake ya mambo ya nje.
Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock atakutana katika nyakati tofauti na mawaziri wa mambo ya nje wa Azerbaijan na Armenia, kabla ya kuandaa mkutano wa pamoja na wote.
Miongoni mwa masuala tete kati ya mataifa hayo Jirani ni ukosefu wa maelewano kuhusu mpaka kati yao, huku kila upande ukishikilia viunga vidogo vinavyozungukwa nae neo la mwingine.
Soma: Azerbaijan na Armenia zatuhumiana kushambuliana mpakani
Mazungumzo hayo yanayofanyika kwa siku mbili, yamejiri miezi mitano tangu Azerbaijan kuchukua udhibiti wa jimbo la Nagorno Karabakh lililokuwa linakaliwa na jamii ya Waarmenia, hatua iliyosababisha maelfu ya watu wa jamii hiyo kukimbia.
Kwa miongo mingi, Marekani, Umoja wa Ulaya na Urusi zote zimejaribu kupatanisha pande hizo mbili