1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yazindua mkakati mkubwa zaidi wa usalama

14 Juni 2023

Serikali ya Ujerumani inapanga kukabiliana na changamoto za mfumo wa dunia unaozidi kuyumba kwa sera ya usalama jumuishi iliyoainishwa hii leo, katika mkakati mpya wa usalama wa taifa.

Deutschland | Kabinett beschließt Nationale Sicherheitsstrategie
Picha: Fabrizio Bensch/REUTERS

Hatua hiyo ni mkakati wa kwanza kabisa wa usalama wa taifa wa Ujerumani, uliozinduliwa wakati ambapo mazingira ya usalama ni ya wasiwasi, kutokana na vita vya Urusi dhidi ya Ukraine na kuongezeka kwa ushindani wa kijiografia kati ya China na Marekani.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, akiwasilisha mpango huo uliopitishwa na baraza la mawaziri siku ya Jumatano, alisema kusudio lake ni kulinda usalama wa raia na kutoa mchango kwenye usalama wa Ulaya:

"Pamoja na mabadiliko yote, bado ni jukumu kuu la serikali kuhakikisha usalama wa raia wake bila maelewano, kwa sababu bila usalama hakuwezi kuwa na uhuru, utulivu na ustawi."

Lengo la mkakati huo  ni kuhakikisha kuwa njia na zana zote zinafanya kazi pamoja ili kuimarisha usalama wa Ujerumani dhidi ya vitisho kutoka nje.

Mkakati huu utahusisha maeneo yote muhimu ya kisera pamoja na watendaji, kuanzia ulinzi wa muungano na wa kitaifa, hadi ulinzi wa miundombinu ya kiufundi na mtandao, pamoja na usalama wa anga hadi malighafi, nishati na usalama wa chakula.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW