1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNamibia

Uji wa sumu waua watu 13 wa familia moja, Namibia

31 Mei 2023

Watu 13 wa familia moja wamekufa nchini Namibia baada ya kunywa uji ambao maafisa wanaamini ulikuwa na sumu.

Ghee gereinigte Butter Produkt Gesundheit Nahrungsmittel Fett
Picha: picture-alliance/dpa/Creative Touch Imaging

Shirika la Utangazaji la Nambia, NBC limeripoti kuwa uji huo ulichanganywa na kitu kilichochacha kilichobaki kutoka kwenye kinywaji cha pombe kilichotengenezwa nyumbani. Kwa mujibu wa NBC, watu wengine wanne wako katika hali mbaya na wamelazwa hospitali. Likiinukuu wizara ya afya, shirika hilo la utangazaji limesema takribani watu 20 walikunywa uji huo wenye sumu baada ya kuchanganywa na mabaki ya bia ya kutengenezwa nyumbani. Wahanga wana kati ya umri wa miaka miwili hadi 33. Tukio hilo limetokea katika jimbo la Kavango Mashariki, kaskazini mashariki mwa Namibia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW