1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Ujumbe wa Afrika wakutana na Putin kuhusu mzozo wa Ukraine

18 Juni 2023

Ujumbe wa viongozi wa Afrika umemtolea wito rais wa Urusi Vladimir Putin kuanzisha mazungumzo ya amani na Ukraine wakati walipokutana naye.

Viongozi wa Afrika mjini St. Petersburg I Putin
Ujumbe wa Afrika katika mazungumzo yao na Vladimir PutinPicha: Pavel Bednyakov/RIA NOVOSTI/AFP

Ujumbe wa viongozi wa Afrika umemtolea wito rais wa Urusi Vladimir Putin kuanzisha mazungumzo ya amani na Ukraine, wakati walipokutana na kiongozi huyo mjini St. Petersburg.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amenukuliwa akisema wana imani kubwa kwamba huu ni wakati muafaka kwa pande zote kuanza mazungumzo na kumaliza vita vinavyoendelea nchini Ukraine, huku rais wa Comoro Azali Assoumani ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, akihimiza kuanza mchakato wa makubaliano ya amani.

Hata hivyo, Putin aliyeivamia Ukraine Februari 2022, kwa mara nyingine ameilaumu Ukraine kwa kutokuwepo kwa mazungumzo hayo ya amani.

Ujumbe huo ambao pia una wawakilishi kutoka Misri, Senegal, Zambia, Congo na Uganda umesema umeandaa mpango wenye pointi 10, ambao ni sehemu ya mkakati wa amani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW