1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Kikosi cha AU chakamilisha awamu mpya ya kuondoka Somalia

3 Februari 2024

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, kimesema jana Ijumaa kwamba awamu ya pili ya uondoaji askari wake wapatao 3,000 imekamilishwa baada ya uchelewaji wa miezi minne.

Uganda Kampala | Mkutano kuhusu Somalia
Mkutano wa ngazi ya juu wa ATMIS ukijadili uondakaji Somalia, Aprili 27, 2023.Picha: Ministry foreign affairs Uganda

Kufuatia kurudi nyuma katika mafanikio yake dhidi ya waasi wenye uhusiano na Al-Qaeda, serikali ya Mogadishu ilikuwa imeomba "usimamishaji wa kiufundi" wa miezi mitatu katika uondoaji uliopangwa kutekelezwa ifikapo Septemba mwaka jana.

"Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS)... kimekamilisha Awamu ya Pili ya kupunguza idadi ya wanajeshi, ambayo ilihusisha kupunguza idadi ya wanajeshi na wanajeshi 3,000," kilisema kikosi hicho katika taarifa yake.

ATMIS ilikabidhi vituo saba vya uendeshaji kwa serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa na kufunga nyingine mbili.

"Hivi karibuni tutaanza maandalizi ya awamu inayofuata, Awamu ya Tatu, ili kupunguza idadi yetu kwa wanajeshi 4,000 mwezi Juni,” alisema Luteni Jenerali Sam Okiding.

Soma pia: Ujumbe wa AU Somalia waanza kuwaondoa wanajeshi wake

Awamu mbili za kwanza za uondoaji zilishuhudia uondoaji wa jumla ya wanajeshi 5,000. Baadhi ya wanachama 14,600 kutoka Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Uganda bado wametumwa nchini Somalia.

Kikosi cha ATMIS kinapasw akukamilisha uondoaji wa wanajeshi Somalia ifikapo mwishoni mwa 2024.Picha: ATMIS press

Chini ya kalenda ya Umoja wa Mataifa, ATMIS inapaswa kuwa imeondoka kikamilifu nchini Somalia kufikia mwishoni mwa mwaka huu, na kukabidhi majukumu ya usalama kwa vikosi vya ulinzi vya Somalia.

"Hivi karibuni tutaanza maandalizi ya awamu inayofuata, Awamu ya Tatu, ili kupunguza idadi yetu kwa wanajeshi 4,000 mwezi Juni,” alisema kamanda wa ATMIS Luteni Jenerali Sam Okiding.

ATMIS ilipewa mamlaka ya kushambulia zaidi ilipochukua nafasi ya kikosi kilichotangulia cha AMISOM mwezi Aprili 2022, kilichoanzishwa mwaka wa 2007 kusaidia serikali dhaifu ya Somalia dhidi ya uasi wa wapiganaji wa itikadi kali.

Soma pia: Wasiwasi watanda Somalia kuondoka kwa kikosi cha Umoja wa Afrika

Al-Shabaab walitimuliwa kutoka katika miji na miji mikuu ya Somalia mwaka wa 2011-2012, lakini wanasalia kudhibiti madaraka katika maeneo makubwa ya vijijini.

Inaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya maeneoo ya usalama na kiraia, ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu, licha ya mashambulizi ya serikali, mashambulizi ya anga ya Marekani na vikosi vya Umoja wa Afrika vilivyoko ardhini.

Chanzo: AFPE

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW