Ujumbe wa haki za binaadamu wa UM waanza uchunguzi juu muaji ya Uzebekistan
15 Juni 2005Bishkek:
Ujumbe wa haki za binaadamu wa Umoja wa mataifa , umewasili katika Jamhuri ya Kyrgystan, kuchunguza machafuko ya hivi karibuni katika nchi jirani ya Uzbekistan. Ujumbe huo wa maafisa wa ngazi ya juu kutoka Ofisi ya kamishna wa Shirika la haki za binaadamu la Umoja wa mataifa, utakuweko huko kwa muda wa siku 10, kuwahoji walioshuhudia matukio hayo pamoja na watu wengine wenye taarifa muhimu. Kuanzia Mei 12 hadi 14, machafuko katika mji wa Andijan katika Jamhuri ya Uzbekistan yalisababisha vifo vya watu karibu 800- kwa mujibu wa Jumuiya zinazopigania haki za binaadamu , ambapo serikali inadai waliouwawa ni 173 . Rais Islam Karimov wa Uzbekistan ameukataa wito wa Umoja wa Ulaya, kutaka paundwe tume huru ya kimataifa ,kuchunguza matukio hayo.