1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa maafisa wa Marekani waitembelea Niger

13 Machi 2024

Ujumbe wa Marekani wa maafisa wake waandamizi umeitembelea Niger jana Jumanne na kukutana na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo. Ziara hiyo inalenga kurudisha mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Niger | Tchiani
Kiongozi wa kijeshi wa Niger Abdourahamane TchianiPicha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Ujumbe wa Marekani wa maafisa wake waandamizi umeitembelea Niger jana Jumanne na kukutana na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo. Hayo yameelezwa kupitia kituo cha televisheni ya taifa ya Niger.

Ziara hiyo inaonesha inalenga kurudisha mahusiano baada ya viongozi wa kijeshi nchini Niger kumuondowa rais aliyekuwepo madarakani na kujisogeza karibu zaidi na Urusi.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na Niger, Ujumbe huo wa Marekani uliomjumuisha naibu waziri wa mambo ya nje anayehusika na masuala ya Afrika,Molly Phee ulikutana na waziri mkuu wa Niger mjini Niamey.

Awali wizara ya mambo ya nje ya Marekani,ilisema jenerali Michael Langley,ambaye ni kamanda wa kamandi ya Marekani barani Afrika,alikuwa pia sehemu ya ujumbe huo ulioko Niger hadi leo Jumatano.