Ujumbe wa viongozi wa Afrika wajiandaa kwenda Moscow na Kiev
22 Mei 2023Ujumbe huo unalenga pia kujadili masuala tete kuhusu namna Urusi inayokabiliwa na vikwazo vingi inavyoweza kupokea malipo ya usafirishaji mbolea inayohitajika zaidi barani Afrika. Hayo yameelezwa na mjumbe muhimu aliyesaidia kufanikisha mazungumzo hayo kupitia mahojiano aliyofanyiwa na shirika la habari la Associated Press.
Jean-Yves Olivier, msuluhishi wa kimataifa ambaye amekuwa akifanya kazi kwa miezi sita kuandaa mazungumzo hayo amesema viongozi wa Afrika pia watajadili masuala mengine kadhaa yanayohusiana na hatua za kulegezwa vizuizi vya meli za usafirishaji nafaka kutoka nchini Ukraine kufuatia vita vinavyoendelea.
Soma pia: Viongozi wa Afrika kutatua mzozo wa Ukraine
Kadhalika watalitazama suala la uwezekano wa ubadilishanaji wafungwa. Kwa mujibu wa Olivier mazungumzo hayo huenda yakafanyika mwezi Ujao wa Juni.