1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Ujumbe wa wabunge wa Ujerumani wawasili Taiwan

9 Januari 2023

Ujumbe wa wabunge wa Ujerumani umewasili Taiwan mapema leo kwa ziara ya siku nne wakati ambapo mivutano inaongezeka katika eneo hilo.

Deutsche Delegation in  Taiwan
Picha: Chia-Chun Yeh/DW

Ujumbe huo unaoongozwa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya bunge la Ujerumani, Bundestag, Marie-Agnes Strack Zimmerman, umewasili wakati ambapo wizara ya ulinzi wa taifa ya Taiwan imesema imeona ndege 57 za kivita kutoka China katika anga yake katika kipindi cha saa 24.

Wizara hiyo imesema ndege 28 kati ya hizo zimeuvuka mpaka usio rasmi wa China na Taiwan.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imeukaribisha ujumbe huo wa Ujerumani utakaofanya kikao na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen na Waziri Mkuu Su Tseng-chang miongoni mwa maafisa wengine wa ngazi ya juu serikalini.

Tangu Oktoba, Ujerumani imeonyesha mshikamano na Taiwan kwa kutuma mara tatu ujumbe wa wabunge.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW