1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukaguzi wa mipakani kuendelea Ujerumani

10 Oktoba 2024

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Nancy Faeser amesema Ujerumani itaendelea na udhibiti wa mipaka yake hadi Ulaya itakapopata suluhisho la uhamiaji haramu.

Deutschland Innenministerin Nancy Faeser
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Faeser amesema kipaumbele chake kitakuwa kutekelezwa kwa sera ya Umoja wa Ulaya ya uhamiaji na hifadhi, inayoakisi sheria kali mpya za Umoja huo katika kushughulikia sera ya uhamiaji.

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Luxembourg kujadili usimamizi wa

uhamiaji huku serikali zikikabiliwa na shinikizo linaloongezeka kutoka kwa wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia katika kushughulikia suala hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW