Ukahaba watishia maisha ya watoto Kenya
20 Desemba 2006Utafiti huo ulidumu kwa mwaka mmoja katika mkoa wa pwani na kudhihirisha kuwa asilimia 30 ya wasichana wadogo wanahusika na vitendo vya ukahaba.
Utafiti huo uliofanyika katika wilaya za Kwale,Kilifi,Malindi na Mombasa ulibaini kuwa takriban wasichana alfu 15 wanahusika na ukahaba vilevile wengine alfu 2 wakijumuisha vijana wanahusika na shughuli hiyo kila siku.
Utafiti huo unaelezea ukubwa wa tatizo hilo na athari zake hasa katika watoto wanaonyanyaswa kijinsia katika eneo la pwani nchini Kenya.Ukahaba unakiuka haki za watoto katika eneo hilo aidha kuweka bayana matatizo yanayowakumba watoto nchini Kenya.
Kulingana na ripoti hiyo matatizo ya pesa na umasikini ndio vyanzo vya shughuli hiyo ya ukahaba hasa kwa watoto.Utafiti huo aidha umevumbua kuwa watoto kutoka maeneo mengine ya nchi mbali na yale ya pwani nao huhusika kabla kuwasili.
Kwa mujibu wa mwandishi wa ripoti hiyo Sara Jones wengi wao hawatumii mipira ya kondom.