1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Ukame Pembe ya Afrika wasababisha njaa kwa watu milioni 13

24 Februari 2022

Maeneo makubwa ya ardhi, kuanzia kusini mwa Ethiopia hadi kaskazini mwa Kenya na Somalia yanakabiliwa na ukame mbaya uliowaacha watu milioni 13 wakikabiliwa na baa la njaa. Ulimwengu wa mifugo pia umeathiriwa pakubwa.

Dürre Hungersnot Afrika Flash-Galerie
Picha: picture alliance/dpa

Katika maeneo hayo ambako watu wanaishi hasa kwa shuguli za kilimo na ufugaji, misimu mitatu ya mbua tangi mwishoni mwa 202 imekuwa ikishuhudia mvua chache sana, na hali hii ilichochewa na uvamizi wa nzige walioharibu mazao kati ya 2019 na 2021.

"Watu wa Pembe wanachangia asilimia nne ya idadi jumla ya watu duniani, lakini kanda hiyo inawakilisha asilimia 20 ya watu ambao wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakukala," alisema Michael Dunford, mkurugenzi wa kanda wa kanda ya Afrika Mashariki wa shirika la chakula duniani, WFP, mapema mwezi Februari.

Soma pia: UN: Watu milioni 13 wanakabiliwa na njaa kubwa katika eneo la Pembe ya Afrika

Kwa muhibu wa shirila hilo la Umoja wa Mataifa, watu milioni 5.7 wanahitaji msaada wa chakula kusini na kusini-mashariki mwa Ethiopia, wakiwemo watoto na kina mama nusu milioni wanaokabiliwa na tatizo la utapiamlo.

Raia wa Ethiopia wakipanga foreni kupatiwa chakula cha msaada katika zoni ya Shinite.Picha: Mulugeta Ayene/AP/picture alliance

Mashariki na kaskazini mwa Kenya, ambako rais alitangaza hali ya janga la kitaita mwezi Septemba kwasababu ya ukame, watu wengine milioni 2.8 wanahitaji msaada.

Nchini Somalia, idadi ya watu walioainishwa kama walio na njaa kali, huenda ikapanda kutoka milioni 4.3 hadi milioni 4.6 kufikia mwezi Mei, iwao hatua za haraka hazitachukuliwa. Mamlaka nchini humo zilitangaza "hali ya dharura ya kiutu" mnamo mwezi Novemba.

"Utapiamlo umefikiwa ngazi ya mzozo," alisema Victor Chinyama, msemaji wa shirika la kimataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, nchini Somalia. "Wakati wa kuchukuwa hatua ni sasa."

Soma pia: Ukame waleta athari jimboni Marsabit nchini Kenya

"Iwapo utasubiri hadi mambo yawe magumu au hadi njaa itangazwe, huenda itakuwa imechelewa," alionya. Mnamo mwaka 2017, hatua za mapema na kiutu zilizuwia njaa katika taifa hilo linalokabiliwa na matatizo.

Lakini mwaka 2011, watu 260,000 -- nusu yao wakiwa watoto wa chini ya umri wa miaka sita -- walikufa kutokana na njaa, kutokana kwa sehemu na jamii ya kimataifa kutochukua hatua, kwa mujibu wa UN.

Guyo Gufu, mfugaji kutoka kabila la Gabra, akiwa amesimama karibu na mizoga ya mifugo yake katika kaunti ya Marsabit, Kenya, Januari, 22, 2022.Picha: BAZ RATNER/REUTERS

Kwa sasa, maombi ya UN ya kiasi cha dola bilioni 1.46 kwa ajili ya Somalia yameitikiwa kwa asilimia 2.3 tu ya lengo.

Mbali na madhara mabaya kwa watu walioathirika, uhaba wa maji na ardhi ya malisho ni chanzo cha mzozo pia, hasa miongoni mwa wafugaji. Ukamse huo unatishia ulimwengu wa wanyama.

Ng'ombe, ambao ni chanzo muhimu cha riziki katika kanda hiyo, wanakufa kwa wingi. Nchini Kenya pekee, mifugo wapatao milioni 1.5 walikufa katika miezi mitatu ya mwisho ya 2021, kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO.

Chanzo: AFPE